Mlinzi wa kati wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Yanga
Benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha Nasreddine Nabi limeonyesha kuwa na imani na beki huyo kisiki na hivyo kumuidhinisha aendelee kubaki kikosini
Msimu uliomalizika haukuwa mzuri sana kwake kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimuandama mara kwa mara
Kwa sasa amepona majeraha hayo, yuko tayari kuwania nafasi kwenye safu ya ulinzi wa kati ambayo inawajumuisha Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Yannick Bangala
ADVERTISE HERE