Kiungo fundi wa Yanga, Aboubakar Salum 'Sure Boy' amesema kwa aina ya usajili uliofanyika mpaka sasa, msimu ujao watakuwa na timu bora zaidi
Aidha, Sure Boy maarufu 'Babu Kaju' amekiri kwamba atahitaji kufanya kazi ya ziada kutetea namba yake lakini anaamini timu hiyo itafanya vizuri zaidi kwenye mashindano yote kuliko misimu iliyopita wakianza na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, Agosti 13.
"Sina hofu yoyote kwa ujio wa wachezaji wapya zaidi wananipa morali ya kupambana zaidi, uwezo nilionao ukichanganya na uzoefu wa Ligi sina sababu ya kuhofia, nina imani na kipaji changu"
"Naheshimu sajili zote, naamini utakuwa chachu ya kufanya vyema na bora kwetu. Kuhusu kucheza, kila mmoja ana umuhimu wake kwa nafasi yake. Nina uhakika wa kucheza najiamini nina kipaji, nimetoka Azam FC vikosi vingi vilipangwa wakiniondoa lakini nimetua nimecheza," Sure Boy amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti
Sure Boy amesema anaamini watakuwa na timu bora yenye ushindani na wataendeleza pale walipoishia na watakuwa na matokeo mazuri ndani na nje kutokana na nafasi waliyoipata kushiriki mashindano ya Afrika.
Yanga imeongeza nyota wanne wa Kimataifa kwenye kikosi huku mwingine akisubiri kutambulishwa
Lazarus Kambole, Bernard Morrison, Lomalisa Mutambala na Gael Bigirimana wakati kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki akisubiri kutambulishwa