Kama ilivyokuwa msimu uliopita, msimu mpya wa 2022/23 ambao utatimua vumbi kuanzia August 17, Wananchi watafungua pazia kwa mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Simba
Mchezo huo utapigwa August 13 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mwaka jana Wananchi walianza kuweka kabatini Ngao ya Jamii, kisha wakachukua ligi kuu na wakahitimisha na kombe la FA
Bado hawajatosheka! wanataka IRUDIWE tena. Usajili makini uliofanywa na Yanga unawapa jeuri na sababu ya kurudia mafanikio waliyopata msimu uliopita
Hiyo August 13 Simba watachagua wenyewe timu ipi ianze, kwani Wananchi wamoto katika kila nafasi...!

AU HIKI?

ADVERTISE HERE