Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema leo wachezaji wataanza kurejea jijini Dar es salaam tayari kuanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya
Bumbuli amesema kesho Jumatatu wataweka hadharani wapi wanakwenda kuweka kambi
Amesisitiza maamuzi ya kambi hiyo yatazingatia muda uliobaki ili kujiandaa na matukio muhimu, Wiki ya Mwananchi na mechi ya Ngao ya Jamii
"Wachezaji tuliwapa likizo ya siku (15), leo (jana) ndio likizo imemalizikia, kuanzia kesho (leo) Wachezaji wataanza kuwasili kambini"
"Nimesikia watu wakisema kuhusu kambi ya Yanga, acha waendelee kusema, Jumatatu tutawajuza wapi tutaenda kuweka kambi, nje ya nchi au hapahapa Dar es Salaam"
"Maamuzi ya wapi tutaweka kambi yatazingatia muda uliobaki ili kujiandaa na matukio muhimu, Wiki ya Mwananchi na mechi ya Ngao ya hisani," alisema Bumbuli
Aidha Bumbuli amebainisha kuwa wachezaji ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa wao wataripoti kambini mwishoni mwa mwezi huu
"Kuna Wachezaji nane wako kwenye kwenye timu za taifa, kuanzia Julai 28 hadi Julai 31 tunatarajia wataripoti kambini"