TFF yafungia viwanja saba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jul 2022
TFF yafungia viwanja saba

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetaja viwanja saba ambavyo vimekosa sifa za kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/2023

Katika tathimini iliyofanywa na TFF wamebaini uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Ilulu Lindi, Usharika (Kilimanjaro), Mabatini (Pwani), Sokoine (Mbeya), Jamhuri (Dodoma) na Nyankumbu Girls (Geita).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya habari ya mawasiliano ya Bodi ya Ligi imethibitisha kuwa kwa mujibu wa kanuni za ligi na sheria namba moja kati ya 17 za mpira wa miguu viwanja hivyo vimekosa sifa katika baadhi ya maeneo.

Walitaja maeneo hayo kuwa ni eneo la kuchezea kutokuwa tambalale na kukosa nyasi za kutosha, ubovu katika uzio wa kutenganyisha mashabiki na eneo la kuchezea, jukwaa kuu kukosa ubora ikiwemo ubovu wa paa.

Pia vyumba vya kuvalia nguo waamuzi na wachezaji vimekosa sifa za ukubwa stahiki pamoja na feni au AC kwaajili ya upatikanaji wa hewa ya kutosha, upatikanaji wa majisafi na ya kutosha muda wote, upatikanaji umeme na uwepo wa vyoo safi na vya kisasa.

Pia kukosekana kwa chumba cha mawasiliano, kukosekana kwa chumba cha madaktari kwaajili ya huduma ya kwanza, kukosekana kwa chumba kwaajili ya maofisa wa mchezo, kukosekana kwa mabenchi ya ufundi bora na yenye uwezo wa kuruhusu watu wasiopungua 17 kukaa, kukosekana kwa majukwaa kwaajili ya watazamaji na uwepo wa mabango au picha za matangazo zisizotambulika na TFF au TPLB.

Bodi ya Ligi imezitaka klabu zinazotumia viwanja hivyo kuhakikisha vinarekebishwa ili kukidhi mahitaji ya kikanuni kabla ya kuanza msimu wa ligi kuu 2022/23

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
26m ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
3h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
8h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’