Yanga yaomba ITC za nyota wapya mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jul 2022
Yanga yaomba ITC za nyota wapya mapema

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wamejipanga kuhakikisha wachezaji wapya wanapata vibali mapema ili washiriki michuano ya ligi ya mabingwa ambayo hatua ya awali itaanza mwezi Septemba

Bumbuli amesema tayari wamepata ITC za baadhi ya wachezaji wakitarajiwa kupata vibali vya wachezaji wote ndani ya muda

"Tunafahamu dirisha la usajili CAF linafungwa August 15, tuko makini kuepuka yale yaliyotokea msimu uliopita"

"Katika wachezaji tuliowasajili, Bernard Morrison hahitaji ITC kwa sababu alikuwa akicheza hapa hapa Tanzania, hatuna wasiwasi kupata ITC za Lazarus Kambole na Gael Bigirimana, tunaendelea kufuatilia ITC za Joyce Lomalisa na Stephane Aziz Ki ambazo pia tutazipata bila ya wasiwasi wowote"

"Msimu uliopita tulipata changamoto kupata ITC ya Khalid Aucho ambaye alikuwa na kesi FIFA dhidi ya timu yake ya zamani na wachezaji wetu kutoka DR Congo Fiston Mayele na Djuma Shabani. Hakukuwa na makosa yoyote upande wetu, lakini wakati huu tumejipanga kuhakikisha tunamaliza kila kitu mapema," alisema Bumbuli

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
41m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’