Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kila mchezaji katika kikosi chake atapaswa kupambana ili kupata nafasi ya kucheza
Nabi amesema wanapoanza maandalizi ya msimu wachezaji ambao watakuwa tayari ndio watakaoingia katika kikosi chake na hataangalia nafasi zao katika msimu uliopita
Nabi anayetarajiwa kutua nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, amesema usajili uliofanyika utawaongezea ubora lakini akasisitiza ni lazima kila mchezaji aipambanie nafasi yake uwanjani
"Ujio wa hawa wapya tunaweza kusema tutakuwa na timu bora zaidi lakini mapema niseme kitu kwa wachezaji wangu, kila mmoja anatakiwa kujiandaa kiakili tunaweza kuwa na mabadiliko makubwa ya timu hii, "alisema Nabi
Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji watano wa kigeni Lazarus Kambole, Bernard Morrison, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana na Stephane Aziz Ki
Nyota wote wana uzoefu wa michuano ya Kimataifa ambapo kama wote wataingia katika kikosi cha kwanza ina maana kuwa wachezaji watano watawapisha