Klabu ya Yanga imethibitisha kuachana na nyota wawili wa kigeni Chico Ushindi na Yacouba Songne
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wamechukua uamuzi huo ili kukidhi kanuni za usajili wa ndani ambazo zinawataka wabaki na wachezaji 12

"Mwezi Januari 2022, tulimchukua Chico kwa makubaliano maalum pale TP Mazembe lakini kwa mapendekezo ya benchi la ufundi, tumeamua kumrejesha katika klabu yake ya zamani, TP Mazembe"
"Mchezaji wa pili ni Yacouba Songne. Kwa hali yake imeonekana bado anahitaji muda aendelee kuimarika hivyo tutakaa nae chini, tuone ni jinsi gani tunaweza kumsaidia wakati akiendelea kuimarika," alisema Manara
Nyota 12 wa kigeni ambao wataitumikia Yanga msimu ujao ni Djigui Diarra, Djuma Shabani, Joyce Lomalisa, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Gael Bigirimana na Jesus Moloko
Wengine ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Stephane Aziz Ki, Lazarus Kambole na Bernard Morrison