Klabu ya Yanga leo imemtambulisha rasmi aliyekuwa msemaji wa Mbeya City, Dismas Ten kuwa Afisa Habari wa Yanga.
Akimtambulisha bosi huyo mpya wa kitengo cha habari, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema huo ni utekelezaji wa moja ya mikakati ya klabu kuunda upya kitengo cha Habari na Mawasiliano.
Ten amekuwa msemaji wa Mbeya City kwa misimu miwili iliyopita na mkataba wake wa kuitumikia Mbeya City umemalizika mwezi Juni.
Ten anachukua nafasi ya Jerry Murro aliyekuwa amefungiwa na TFF, adhabu yake imemalizika.
Kabla, nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Godlisten Anderson Chicharito kama kaimu afisa habari ambaye sasa ataendelea kumsaidia Dismas Ten.
Katika hatua nyingine, Mkwasa amewataka mashabiki wa Yanga kuwa na utulivu. Uongozi wa Yanga utaendelea kutoa taarifa kwao kila mda muafaka.

ADVERTISE HERE