Leo Alhamisi, Julai 21 2022 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atazungumza na waandishi wa habari za Michezo
Huenda ajenda ya Mkutano huo ikawa kesi inayomkabili Msemaji wa Yanga Haji Manara dhidi ya Rais wa TFF Wallace Karia baada ya sintofahamu iliyojitokeza kwenye mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union uliopigwa Julai 02 uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Wiki iliyopita, Manara aliitwa na kuhojiwa kwenye Kamati ya Maadili

ADVERTISE HERE