Ndio kauli ya Haji Manara kuelekea Wiki ya Mwananchi ambayo itaanza August 01 na kuhitimishwa August 06 pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Manara amesema wamejipanga kufanikisha Tamasha kubwa zaidi la Wananchi kuliko wanavyofikiria!
Licha ya kufungiwa kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka miwili, Manara hazuiwi kufanya shughuli zake binafsi nje ya uongozi wa Yanga ambao ni Wanachama wa TFF
Manara hazuiwi kuwa shabiki wa klabu anayoipenda kwa sasa, YANGA. Jambo pekee ambalo hatalifanya ni kuwa msemaji rasmi wa Yanga
Kazi ya usemaji itaendelea kufanywa na Afisa Habari Hassan Bumbuli...!
ADVERTISE HERE