Yanga hii ina watu aisee

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2022
Yanga hii ina watu aisee

Usajili uliofanywa na Yanga katika dirisha la usajili umeifanya iwe na wachezaji wengi ambao wanaweza kuipa faida kubwa katika mbio za ubingwa mbele ya washindani wao wakuu Simba na Azam.

Katika kikosi cha wachezaji 30 ambao timu hizo kila moja itawasajili kwa ajili ya Ligi Kuu na michuano mingine msimu ujao, Yanga imepiga bao la kisigino kwa kuwa na nyota tisa wenye uwezo wa kucheza katika nafasi nyingi tofauti uwanjani

Wachezaji hao ni Kibwana Shomari, Dickson Job, Yannick Bangala, Aziz Ki, Lazarous Kambole, Salum Abubakar, Feisal Salum, Bernard Morrison na Farid Musa.

Licha ya kila nafasi katika kikosi cha Nabi kuwa na wachezaji wawili au watatu wanaomudu vyema kuicheza, uwepo wa nyota hao viraka unaifanya Yanga kuwa na uhakika wa kumudu msimu mzima na kushiriki vyema katika michuano mingi tofauti hata ikitokea baadhi yao kuwa majeruhi na wengine kutokuwa na kiwango kizuri kwa wakati husika.

Uwepo wa Job, Kibwana na Bangala wanaoweza kucheza katika nafasi tofauti za ulinzi kwa ufanisi nmkubwa, unaipa Yanga jeuri katika msimu ujao wa kuwa na ukuta imara hata pale inapotokea mmoja kati ya mabeki wengine, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Ibrahim Baka, Djuma Shaban na David Bryson anapokosekana.

Wakati Job akimudu kucheza nafasi ya beki wa kati, beki wa kulia na kiungo mkabaji, Bangala anaweza kucheza nafasi zote uwanjani isipokuwa kipa huku Kibwana akionyesha kumudu nafasi ya beki wa kulia, kushoto na hata winga

Ukimuondoa Bangala ambaye mara kwa mara amekuwa akitumika kama kiungo, viungo wengine wa Yanga wenye kuipa wigo mpana wa uteuzi wa kikosi benchi lao la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi iwapo baadhi ya wachezaji watakosekana ni Feisal, Aziz Ki, Farid Musa na Sure Boy.

Feisal na Sure Boy kila mmoja anaweza kucheza nafasi ya kiungo namba sita, nane, winga na namba 10 wakati Ki anamudu nafasi ya winga, kiungo mshambuliaji na hata kucheza kama mshambuliaji wa kati.

Farid ameonyesha uwezo mkubwa wa kucheza kama beki na winga wa kushoto, kiungo namba 10, pia anaweza kucheza hata namba nane.

Katika ushambuliaji, Yanga ina Morrison na Kambole ambao kila mmoja anamudu kucheza nafasi ya winga, mshambuliaji wa kati na pia namba 10

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’