Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Somalia katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya CHAN inayohusu wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya Afrika
Fainali za michuano hiyo zitafanyika mwakani huko Algeria
Somalia ndio wenyeji wa mchezo huo lakini wamechagua kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na kukosekana kwa utulivu katika nchi yao
Timu hizo zitarudiana hapo dimba la Mkapa Julai 28 katika mchezo wa pili ambao Tanzania itakuwa mwenyeji
ADVERTISE HERE