Kocha Mkuu wa Yanga Mohammed Nasreddine Nabi leo amekabidhiwa tuzo ya Kocha Bora wa ligi kuu msimu wa 2021/22
Katika msimu uliopita, Nabi aliingoza Yanga kutwaa mataji matatu ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Yanga ilishinda mataji hayo pasipo kupoteza mchezo wowote
Nabi aliondoka nchini baada ya mchezo wa fainali ya FA hivyo hakushiriki hafla ya utolewaji tuzo hizo iliyofanyika Julai 07 2022
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alipokea tuzo hiyo kwa niaba yake
Nabi anakiongoza kikosi cha katika maandalizi ya msimu ujao yanayoendelea Avic Town, Yanga ikijipanga kurudia mafanikio waliyopata msimu uliopita
ADVERTISE HERE