Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji watatu waliotajwa na Shirikisho la Soka Ivory Coast kuwania tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu katika msimu wa 2021/22
Akiitumikia Asec Mimosas, Aziz Ki alihitimisha msimu uliopita na mabao 10 pia akitoa pasi sita za mabao
Katika kinyang'anyiro hicho, anachuana na mshambuliaji kinda Karim Konate na Traore Yssf
Aziz Ki alichuana na Konate katika tuzo ya mchezaji bora wa msimu kwa timu ya Asec na Konate kushinda tuzo hiyo
Konate pia ana nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ivory Coast, akimaliza msimu na mabao 27
Tayari Konate amesajiliwa RB Salzburg ya Austria ambayo imemtoa kwa mkopo klabu ya FC Liefering, wakati Aziz Ki akitua Yanga
Aziz Ki anatajwa kuwa usajili ghali zaidi uliofanywa mpaka sasa na klabu za Tanzania katika dirisha la usajili lililofunguliwa Julai 01 likitarajiwa kufungwa August 31