Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele amewanyamazisha wale waliokuwa wakizusha kuwa anacheza kwa Wananchi kwa mkopo
Ni taarifa ambazo zilizushwa na wapo watu walianza kuziamini hasa baada ya tetesi kuwa Mayele amejiunga na Kaizer Chiefs
Baada ya kurejea nchini na kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kuelekea msimu ujao, Mayele amesema ana mkataba na Yanga na msimu ujao atawatumikia mabingwa hao wa nchi
βNimesikia eti wanasema hilikuja Yanga kwa mkopo, sio kwa mkopo nina mkataba hapa,β alisema Mayele
ADVERTISE HERE