Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imesema suala ya wachezaji wa kigeni 12 waliosajiliwa kucheza wote katika mchezo mmoja litapelekwa kwenye kamati husika na huko ndiko hatima yake itaamuliwa, imeelezwa
Ofisa Mtendeji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo amekiri kupokea maoni mbalimbali ya wadau wa mpira wa miguu kwa ajili ya maboresho ya kanuni za Ligi Kuu msimu ujao wa 2022/2023, huku suala ya wachezaji 12 la kigeni likiwa miongoni mwa maoni hayo.
"Ni mapema sana kusema, bado tupo kwenye huo mchakato, tutapeleka kwenye vikao halali vitaamua kwa sababu hili ni jambo la kanuni siyo jambo la Bodi, wala TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), ni la wadau wenyewe, ambao ni klabu, ndiyo wataamua ni namna gani ambavyo wanataka wachezaji wa kigeni 12," alisema Kasongo
Mbali na hayo, ofisa huyo alisema sekretarieti ya bodi hiyo itakutana kesho kupitia na kujidhihirisha maoni yote yaliyotumwa kama yapo sawa na kuyapekeka katika vikao husika.