Kwa Bigirimana tumeokota dhahabu - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2022
Kwa Bigirimana tumeokota dhahabu - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametamba na usajili wa kiungo Gael Bigirimana akibainisha kuwa wamepata mtu hasa

Baada ya kucheza barani Ulaya kwa zaidi ya miaka 10, Bigirimana amesajiliwa na Yanga katika dirisha hili la usajili ikiwa ndio klabu yake ya kwanza kucheza barani Afrika

Wiki moja ya mazoezi imemtosha Nabi kubaini Bigirimana ni mchezaji wa aina gani na upi utakuwa mchango wake kwa Yanga

"Ni mtu aliyekamilika sana, nafikiri uamuzi wake wa kuja hapa Yanga ni kama tumepata dhahabu kubwa ambayo itatupa mabadiliko makubwa katika kikosi chetu"

"Nafikiri sio tu mashabiki wataburudika na ubora wake lakini pia hata wachezaji ambao watamuangalia kuna vitu watajifunza, anavyocheza ndivyo kiungo wa kisasa anatakiwa kucheza, ukiona jinsi anavyokaba na kupiga pasi nafsi yako inatulia," alisema Nabi

Nabi anaendelea kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya kilele cha wiki ya Mwananchi August 06 na msimu mpya wa ligi kuu utakaoanza August 17 ambao utatanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’