Yanga imezindua rasmi wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake itakuwa Jumamosi August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kutakuwa na mchezo maalum baada ya utambulisho wa timu
Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika Serena Hotel mapema leo, Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia tukio hilo, Arafat Haji amesema wamejipanga kufanya tukio kubwa litakalotikisha nchi
Arafat ametangaza kuwa Yanga itacheza na Vipers Fc, mabingwa wa ligi kuu ya Uganda katika kilele cha tukio hilo August 06 pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Benki ya CRDB imejitosha kudhamini tukio hilo ikiungana na wadhamini wengine wa klabu, Sportpesa
Kauli mbiu ya Wiki ya Wananchi mwaka huu ni Byuti Byuti....!
ADVERTISE HERE