Wachezaji saba wa Yanga waliokuwa na majukumu kwenye timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', wanatarajiwa kuripoti kambini Avic Town kuendelea na pre-season
Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Salum Abubakar na Feisal Salum walikuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichofanikiwa kutinga raundi ya pili michuano ya CHAN kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Somalia
Mkufunzi wa Yanga Nasreddine Nabi sasa atakuwa na wachezaji wote kukamilisha maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumamosi ambapo Yanga itacheza na Vipers Fc, mabingwa wa ligi kuu ya Uganda
Jana winga Bernard Morrison aliripoti kambini na moja kwa moja kuanza mazoezi na wachezaji wengine
Kikosi cha Yanga leo asubuhi watakuwa program ya mazoezi ya Gym na jioni kuendelea na mazoezi ya uwanjani, Avic Town