Wapinzani wa Yanga katika kilele cha wiki ya Mwananchi, Vipers Fc wanatarajiwa kutua nchini kesho Alhamisi August 04 tayari kwa Tamasha hilo kubwa la michezo ambalo litafanyika Jumamosi, August 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Vipers ni mabingwa wa ligi kuu ya Uganda, hivyo mchezo huo utakuwa kipimo kuzuri kwa Yanga kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa August 13
Kabla ya kuumana na Vipers, kikosi cha Yanga huenda kikacheza mchezo mmoja pale Avic Town dhidi ya timu ya ligi kuu
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameendelea kukiimarisha kikosi chake sasa akiwa na wachezaji wote baada ya nyota waliokuwa na majukumu timu ya Taifa kuripoti kambini jana
ADVERTISE HERE