Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC msimu wa 2022/23 itaanza kutimua vumbi August 15 ambapo Yanga itashuka dimbani August 16 siku tatu baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa August 13
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Almas Kasongo ameweka hadharani ratiba hiyo ambapo August 15 mechi mbili zitapigwa
Ihefu Fc watakabiliana na Ruvu Shooting na mchezo wa pili ni kati ya Namungo Fc dhidi ya Mtibwa Sugar
August 16 Yanga itakuwa Kilimanjaro kuikabili Polisi Tanzania wakati Singida Big Stars watacheza na Prisons
Mchezo mwingine ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Mbeya City
August 17 itapigwa michezo mingine mitatu; Coastal Union dhidi ya KMC, Simba dhidi ya Geita Gold na Azam fc dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba utapigwa Oktoba 23 saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa
Bodi ya ligi imebainisha kuwa ligi haitasimama wakati wa michuano ya kombe la Dunia, Ligi itamalizika May 27 2023