Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga mliojitokeza kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi kilichofikiwa siku ya jana.
Hakika mmetuheshimisha sana, niwaombe tuendelee kuisapoti timu yetu kwani bila nyie hakuna Yanga.
Pia niwape pole kwa matokeo ya jana, lakini niwatoe hofu, matokeo ya jana ni muhimu sana kwa timu yetu na benchi la ufundi kwa ujumla, wamepata homework ya kwenda kufanya ili kujiandaa na mchezo wa ngao ya jamii, michezo ya ligi na mashindano ya CAF.
Mwisho niwaombe ndugu zangu WanaYanga na waTanzania kwa ujumla tuisapoti serikali yetu, tujitokeze kuhesabiwa, sensa ya watu na makazi ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu
SIMON PATRICK
ADVERTISE HERE