Droo ya hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imefanyika leo ambapo mabingwa wa Tanzania Yanga wataanzia ugenini dhidi ya Zalan ya Sudani Kusini
Mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 09-11 huko Sudani Kusini na mchezo wa marudiano kupigwa jijini Dar es salaam wiki moja baadae
Kama Yanga itafanikiwa kuvuka hatua ya awali, itakutana na mshindi wa mchezo kati ya St George ya Ethiopia dhidi ya Al Hilal ya Sudan
Kwa upande wa watani zao Simba nao wataanzia ugenini dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi ambapo kama watafanikiwa kuvuka hatua hiyo watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Red Arrows ya Zambia dhidi ya Premero Di Agosto ya Angola
ADVERTISE HERE