Pamoja na kuwa hajajumusihwa kwenye kikosi cha wachezaji 12 waliosajiliwa kwa ajili ya ligi kuu ya NBC, mshambuliaji Yacouba Songne anaweza kujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kitakachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Dirisha la usajili wa CAF litafungwa August 15 na timu zinaruhusiwa kusajili mpaka wachezaji 40, hakuna ukomo wa wachezaji wa kigeni
Yacouba ameendelea kufanya mazoezi na Yanga pia anapata nafasi ya kucheza mechi za kirafiki zinazopigwa Avic Town


Licha ya mkataba wake kumalizika, Yanga iliahidi kuendelea kumhudumia ili kuhakikisha anarejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi nane akiwa majeruhi
Kama atamshawishi Nabi huenda akajumuishwa katika kikosi cha CAF na pengine akaonekana tena kwenye ligi pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Disemba