Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliopigwa juzi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Arusha ambako watacheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu huu wa 2022/23
Ni mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumanne, August 16 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Wananchi wameelekea Arusha wakiwa na kikosi kamili kinachowajumuisha nyota wote waioiadhibu Simba siku ya Jumamosi
Yanga ina kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi msimu uliopita katika mchezo waliocheza na Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Bao la Dickson Ambundo liliihakikishia Yanga ushindi muhimu wa bao 1-0
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema wanakwenda Arusha wakiwa na dhamira moja, kupata alama zote tatu katika mchezo huo
Yanga imepania kurejesha taji la ligi kuu Jangwani kama walivyofanya Ngao ya Jamii hapo juzi
Ni msimu mwingine kwa mshambuliaji Fiston Mayele kuwania kiatu cha dhahabu baada ya kukikosa kidogo msimu uliopita akizidiwa bao moja na George Mpole wa Geita Gold