Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/23 imeanza leo kwa michezo miwili kupigwa
Mchezo wa mapema uliopigwa saa kumi jioni uliwashuhudia Ihefu Fc wakikaribishwa tena ligi kuu kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting
Bao la Ally Bilaly liliihakikishia Ruvu Shooting ushindi huo muhimu
Namungo Fc wakitumia uwanja wa Benjamin Mkapa wakatoshana nguvu na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2
Ligi hiyo inaendelea tena kesho Jumanne kwa mabingwa watetezi Yanga kushuka dimba la Sheikh Amri Abeid kuikabili Polisi Tanzania
Mchezo utakaopigwa mapema ni kati ya Singida Big Stars dhidi ya Tanzania Prisons, utapigwa saa nane mchana kwenye uwanja wa Liti, Singida
Saa moja usikui Dodoma Jiji watachuana na Mbeya City
ADVERTISE HERE