Wananchi wako mkoani Arusha ambapo jioni ya leo watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa kwanza wa igi kuu msimu wa 2022/23
Wakiwa ni mabingwa watetezi na mabingwa wa kihistoria wakishinda taji la ligi kuu mara 28, leo wanaianza kampeni ya kusaka ubingwa wa 29
Kikosi cha Kocha Nasreddine Nabi kilitua Arusha mapema jana na jioni wachezaji wakafanya mazoezi yao ya mwisho kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid
Wananchi wataingia katika mchezo huo wakiwa tayari wameweka kibindoni taji la Ngao ya Jamii wakiwachapa watani zao Simba mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi
Mchezo utapigwa kuanzia saa 10 kamili jioni
ADVERTISE HERE