Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wameanza vyema kampeni ya kutetea ubingwa wao baada ya kuichapa Polisi Tanzania mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na nusura Mayele afunge bao sekunde chache tu baada ya mchezo kuanza
Presha kubwa ya Wananchi kwenye lango la Polisi ilipelekea Yanga kupata mkwaju wa penati mapema lakini Mayele akashindwa kuuweka mpira nyavuni
Polisi Tanzania wakafunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 34 kupitia kwa Ally Kipemba baada ya mpira uliookolewa na Mwamnyeto kumgonga na kujaa kimiani
Hata hivyo Yanga ilirejea mchezoni kwa dakika ya 41 kupitia kwa Mayele
Kipindi cha pili kilikuwa cha Yanga, mashambulizi mfululizo kwenye lango la Polisi yalizaa matunda kwenye dakika ya 85 Mwamnyeto akifunga bao la ushindi kwa Yanga
Krosi mahiri kutoka kwa Bernard Morrison ilitua katika mguu wa kulia wa Mwamnyeto ambaye aliujaza mpira kimiani
Ni ushindi wa kwanza msimu huu, Wananchi wakienda kileleni mwa msimamo wa ligi mapemaaa


