Ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga wamepata dhidi ya Polisi Tanzania leo umewafanya waifikie rekodi iliyowekwa na Azam Fc kucheza michezo 38 pasipo kupoteza mchezo wowote
Yanga wanahitaji kutopoteza mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union ili kuweka rekodi mpya ya kucheza mechi 39 pasipo kupoteza
Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo ni April 23 2021 dhidi ya Azam Fc
Kocha Nasreddine Nabi ameendelea kutengeneza takwimu za kutisha katika ligi kuu kwani tangu ajiunge na Yanga, amepoteza mechi moja tu
ADVERTISE HERE