Yanga imepokea mwaliko wa mshambuliaji wake kinda Clement Mziza ambaye anatakiwa na klabu kubwa ya Olympic Marseille ya Ufaransa.
Mkurugenzi wa ufundi wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema tayari Marseille wameshatuma mualiko kwa ajili ya Mziza kwenda kufanya majaribio ya wiki mbili huko Ufaransa
"Huo mualiko upo klabuni viongozi wanaufanyia kazi nafikiri katika majaribio hayo atafanikiwa kwa kuwa nimekuwa naye naona ubora wake kwa umri wake Marseille hawataweza kumuacha"
"Ni mtoto hodari sana ana nguvu na anajua kufunga naona jinsi Tanzania inapata shida katika kuwa na wafungaji wazuri, huyu Clement kama atatunzwa vizuri na kuendelezwa na yeye mwenyewe kujitambua atakuja kuwa mtu bora katika taifa hili,"alisema Zahera
Mziza alikuwa mfungaji bora wa ligi ya vijana iliyomalizika karibuni akiweka kambani mabao matano
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi tayari alishamjumuisha kwenye kikosi chake msimu huu