Mshambuliaji wa Yanga Lazarus Kambole ameanza kushiriki kikamilifu mazoezi na wachezaji wenzake baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua
Wananchi bado hawajamshuhudia Kambole katika kikosi cha Yanga tangu aliposajiliwa na mabingwa hao wa nchi
Kambole alipata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki wakati wa pre-season dhidi ya Namungo Fc
Habari njema ni kuwa ligi imesimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya CHAN, Kambole atakuwa na muda zaidi wa kuimarika na pengine anaweza kuonekana kikosini katika mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kambole alitua Yanga akitokea klabu ya Kaizer Chiefs aliyoitumikia kwa misimu mitatu
ADVERTISE HERE