Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika hatua ya awali dhidi ya St Louis.
Mchezo huo unapigwa leo kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza kwa niaba la benchi la Ufundi kuelekea mchezo huo, Nsajigwa amesema wachezaji wameandaliwa kwa kazi moja tu ya kupata ushindi.
Akizungumzia kuhusu kikosi cha Yanga, Nsajigwa amesema wachezaji wote ambao wamekuwa wakijifua katika kikosi wiki hii wanahali nzuri na wako tayari kwa mchezo huo
"Tutakuwa na wachezaji ambao tupo nao tukifanya nao kazi siku zote pamoja na wale waliojiunga nasi siku mbili tatu zilizopita wote wapo vizuri."
"Lengo letu ni kuibuka na ushindi mnono hapa nyumbani ili kwenye mchezo wa marudiano tukawe na kazi rahisi ugenini," amesema Nsajigwa.
Mchezo huo utaanza saa kumi kamili jioni na utarushwa mubashara na Azam Sport 2 kuwapa fursa wale watakaoshindwa kufika uwanja wa Taifa kuweza kuushuhudia majumbani mwao.

ADVERTISE HERE