Mawindo ya Azam Fc yameanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2022
Mawindo ya Azam Fc yameanza

Kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi inayofuata ya Ligi Kuu dhidi ya Azam FC itakayopigwa Septemba 6, mwaka huu

Meneja wa Yanga Walter Harrison, amesema kuwa wachezaji wote, kasoro wale waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars wamerejea kambini, huku wachezaji walioumia kwenye mechi kati yao dhidi ya Coastal Union, Yannick Bangala na Jesus Moloko wakiendelea vizuri.

"Tuko kwenye mazoezi ya utimamu wa mwili 'gym' ambayo ndiyo tumeanza nayo, kikosi kizima kiko mazoezini kasoro wale tu ambao walikuwa kwenye timu ya taifa. Lengo ni kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu inayokuja dhidi ya Azam FC, lakini siku chache tu baada ya hapo tutakuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati yetu na Zolan FC," alisema Harrison.

Kuhusu Zolan FC, kuomba kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama wao wa nyumbani, alisema hilo lilikuwapo, lakini litatolewa taarifa baadaye kwani linaratibiwa kwa pamoja kati ya viongozi wa klabu yake na wale wa Shirikisho la Soka nchini, TFF.

"Na suala la mechi za kirafiki ni mpaka tuwasiliane na mwalimu atuambie ni aina gani ya timu ambayo anaihitaji, kwa kweli kwa muda uliopo ni lazima kupata mechi ya kirafiki. Kingine ni kwamba majeruhi wetu wanaendelea vizuri, kama utakumbuka tulizalisha majeruhi wawili kwenye mechi dhidi ya Coastal Union, Jesus Moloko na Yannick Bangala"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
57m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’