Pamoja na kuwa Yanga ni kama imefunga hesabu za usajili, Mkurugenzi wa Mashindano Saad Kawemba amesema bado nafasi ya maboresho ipo kama watapokea mapendekezo kutoka kwa benchi la ufundi
Dirisha la usajili wa ndani litafungwa August 31, siku sita zikiwa zimesalia
Saad amesema wanamsikiliza kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi, kama atahitaji maboresho katika dakika hizi za lala salama, watatimiza
"Ni kweli sisi tumeshasajili kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi lakini kama kocha atahitaji mchezaji mwingine katika kipindi hiki awe wa ndani au nje tutamletea," alisema
Yanga inahusishwa na winga wa Singida Big Stars Dario raia wa Brazil aiyesajiliwa na timu hiyo katika dirisha hili la usajili
Hata hivyo kama Yanga itamnasa winga huyo itaweza kumtumia kwenye ligi ya ndani tu kwani dirisha la usajili kwa ajili ya ligi ya mabingwa mechi za mtoano tayari limefungwa
Mchezaji ambaye atasajiliwa sasa klabu italazimika kulipa faini na atatumika kuanzia hatua ya makundi