Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema wanafanya maandalizi makini kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Septemba 06 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni dabi ya Dar es salaam, mechi yenye msisimko nyuma ya mchezo wa watani wa jadi, Yanga na Simba
Nabi amesema amewafuatilia Azam Fc, amebaini ni timu iliyoimarika zaidi ya walivyokuwa msimu uliopita kutokana na usajili mzuri waliofanya
Amesema anafahamu wanakwenda kukutana na timu imara, watahitaji kuwa katika ubora kuweza kupata matokeo mazuri katika mchezo huo
"Niliwaona Azam na naendelea kuwafuatilia, hii sio timu tuliyoifunga mara mbili msimu uliopita, kwa sasa ina kikosi bora sana, imeleta wachezaji bora kabisa ambao naamini watawarudishia matokeo mazuri"
"Tunatakiwa kuwa makini kuanzia katika maandalizi yetu mpaka siku ya mchezo, kuna wakati matokeo yanaweza kuamiliwa na ubora wa wachezaji achilia mbali wana kocha mzuri na watu wengine bora wanaomsaidia kazi," alisema Nabi
Msimu uliopita Yanga ilichukua alama zote sita dhidi ya Azam Fc wakishinda 2-0 dimba la Mkapa na pia kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Azam Complex