Aliekuwa Mgombea ujumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu Yanga kwenye uchaguzi ulioisha hivi karibuni, Benjamjini Mwakasonda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Kairuki
Mwakasonda, Mwanachama wa muda mrefu klabu ya Yanga amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi
Mwakasonda ameshiriki matukio muhimu ya klabu ya Yanga kwa vitendo, alikuwa miongoni mwa waliopitishwa kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji klabu ya Yanga katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mwakasonda mahala pema peponi, AMEN
ADVERTISE HERE