Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' italazimika kwenda kusaka ushindi ugenini nchini Uganda kuweza kufuzu kwa michuano ya CHAN 2023 inayohusisha wachezaji wa ndani baada ya kupoteza mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Tanzania imechapwa bao 1-0 na Uganda mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Licha ya kumiliki mchezo kwa muda mwingi, kosa moja kwenye safu ya ulinzi liliigharimu Stars kwenye dakika ya 86 Uganda wakifunga kupitia shambulizi la kushitukiza
Tanzania itahitaji kushinda angalau mabao mawili nchini Uganda katika mchezo wa marudiano ambao utapigwa Septemba 03
ADVERTISE HERE