Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema ana deni kubwa kwa mashabiki wa timu hiyo kutokana na mapokezi makubwa waliyompatia
Aziz Ki aliyejiunga na Yanga akitokea klabu ya Asec Mimosas, amesema kuna hamasa kubwa ya mashabiki wa soka Tanzania, hilo linamfanya kujiona na deni kubwa kwa Yanga
"Ni mapema sana kuzungumzia soka la Tanzania lakini ninachoweza kusema, watu wanapenda sana mpira hapa. Binafsi bado nina deni kubwa na Yanga, natamani kutimiza ile kiu ya mashabiki wa klabu hii ambayo ipo kwangu na kila mmoja katika timu yetu," alisema Aziz Ki katika mahojiano na Clouds Fc radio
Mchezaji bora huyo wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliopita, ana assist moja kwenye ligi pia akitoa assist moja kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba
Juzi alikuwepo dimba la Mkapa kushuhudia mchezo wa CHAN kati ya Tanzania dhidi ya Uganda na baada ya mchezo huo kumalizika, umati wa mashabiki walimsindikiza mpaka kwenye gari yake huku wakiimba jina lake