Msemaji wa Yanga Haji Manara ameipongeza Kamati ya Saa 72 ya Bodi ya Ligi kwa kuchukua hatua kwa matukio yasiyo ya kiungwana ikiwa ni pamoja na kuiadhibu Yanga kufuatia vitendo vya mashabiki wake kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania
Hata hivyo Manara ameeleza kushangazwa na Kamati hiyo kutochukua hatua yoyote kwa matukio ya hatari waliyofanyiwa wachezaji wa Yanga Salum Abubakar (Mchezo wa Ngao ya Jamii) na Yannick Bangala (Mchezo dhidi ya Coastal Union)
Katika adhabu zilizotolewa na Kamati hiyo, hawakuzungumzia kabisa tukio lililofanywa na Hennock Inonga wa Simba dhidi ya Sure Boy na rafu mbaya iliyofanywa na Mtenje Albano wa Coastal Union dhidi ya Bangala
Kamati imemuadhibu mwamuzi wa mchezo dhidi ya Coastal Union kutokana na tukio la Mtenje lakini inashangaza hawakumchukulia hatua mchezaji aliyefanya tukio lenyewe
Manara amekumbusha matukio ya aina hiyo ambayo yalifanywa na wachezaji wa Yanga msimu uliopita (Dickson Job na Djuma Shabani), waamuzi hawakuyaona wakati wa mchezo lakini wakafungiwa na Kamati baadae