Kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, mashabiki wa Yanga wameaswa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Licha ya kikosi chake kuvuna alama zote sita dhidi ya Azam Fc msimu uliopita, Nabi amesema matokeo hayo hayawapi kiburi na kuamini watashinda mchezo wa kesho pasipo kupambana
Wingi wa mashabiki ni silaha muhimu kwa Yanga katika kuhakikisha alama zote tatu zinapatikana. Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza katika dimba la Mkapa kwenye ligi msimu huu
Viingilio vya mchezo huo;

ADVERTISE HERE