Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anakwenda kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc leo akiwa na kikosi chake kamili
Wachezaji wawili waliokuwa kwenye hatihati ya kukosa mchezo huo mlinda lango Djigui Diarra na mlinzi wa kulia Djuma Shabani nao wako tayari
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kusaka alama tatu ambazo zitawafanya waendeleze rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 kwenye ligi msimu huu
Baada ya kucheza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, mlinda lango Aboutwalib Mshery anaweza kuanza mbele ya Diarra ambaye ndio kwanza amerejea kikosini baada ya kupona majeraha
Djuma, Kibwana Shomari, Yannick Bangala na Dickson Job wanaweza kuanza katika safu ya ulinzi
Khalid Aucho ameanza vyema msimu, akicheza mechi zote kuanzia Ngao ya Jamii, huenda akaanza kwenye eneo la kiungo sambamba na Feisal Salum 'Fei Toto' ambaye kwa sasa amerejeshwa katika nafasi yake ya zamani baada ya ujio wa Stephane Aziz Ki
Baada ya wiki mbili za mazoezi makali pale Avic Town, Bernard Morrison sasa yuko fit na huenda akaanza eneo la winga sambamba na Jesus Moloko aliyepona majeraha aliyopata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union
Aziz Ki na Fiston Mayele bila shaka wataongoza safu ya ushambuliaji kwani wawili hao wameonyesha maelewano mazuri katika michezo iliyopita
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana, Heritier Makambo, Farid Mussa, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Sure Boy na wengine wote wako timamu kuisaidia Yanga kusaka alama tatu mbele ya Azam Fc