Yanga imeendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo kwenye ligi kuu ya NBC sasa wakifikisha siku 500 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam Fc
Yanga imecheza mechi 40 mfululizo pasipo kupoteza mchezo
Azam Fc ilikuwa timu ya mwisho kuifunga Yanga April 25 2021 na nusura wachafue rekodi hiyo ya Wananchi kama sio uhodari wa Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga mabao yote ya Yanga
Wachezaji wa Yanga wanastahili pongezi kwa kupambana kuhakikisha hawapotezi mchezo huo licha ya kutanguliwa mara mbili
Kituo kinachofuata sasa ni mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zalan Fc ambao utapigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex
ADVERTISE HERE