Bado hakuna taarifa juu ya ujio Zalan Fc wa wapinzani wa Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
Mabingwa hao wa Sudan Kusini, jana walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Atlabara Juba na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
Huenda wakawasili nchini leo tayari kuwakabili Yanga siku ya Jumamosi katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa kumi jioni
Zalan Fc wamekuwa na maandalizi mazuri ya pre-season hivyo Yanga watarajie upinzani mkali kutoka kwa mabingwa wenzao wa Sudan Kusini
Wananchi hawapaswi kuingia kwenye propaganda za kuaminishwa kuwa Zalan Fc ni timu dhaifu, sio kweli, wanakuja Tanzania kushindana
ADVERTISE HERE