Msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika unaanza kwa michezo hatua ya awali kuanza kupigwa
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga ni miongoni mwa timu zitakazoshuka dimbani leo kusaka tiketi ya kutinga raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Yanga imepata ahueni kwani watawakabili Zalan Fc ya Sudan Kusini mechi zote mbili zikipigwa hapa Tanzania
Leo Zalan Fc watakuwa wenyeji katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa kumi jioni
Mabingwa hao wa Sudan Kusini walitua kwa mafungu kundi la pili likiwasili majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo
Yanga ina kila sababu ya kupata matokeo dhidi ya Zalan Fc na kusonga mbele raundi ya kwanza
Hata hivyo ni jukumu la benchi la ufundi na wachezaji kuhakikisha matokeo yanapatikana wakianza na mchezo wa leo
Kosa ambalo Yanga hawapaswi kufanya ni kuwadharau wapinzani wao. Bahati mbaya hakuna taarifa sahihi kuhusu Zalan Fc kwani ni timu ambayo wengi wameifahamu baada ya kupangwa na Yanga
Ushindi kwa Yanga katika mchezo wa leo utawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza pale timu hizo zitakaporudiana Septemba 17 hapohapo uwanja wa Mkapa
Kila la kheri Yanga, Kila la kheri Mabingwa wa nchi...!