St George ya Ethiopia imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali, mkondo wa kwanza. Mchezo huo umepigwa leo huko Ethiopia
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo kwenye mchezo wa mkondo wa pili ambao utapigwa huko Sudan
Timu itakayoibuka na ushindi kwenye matokeo ya jumla baada ya michezo yote miwili, itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Zalan Fc
Yanga ni kama imeweka mguu mmoja raundi ya kwanza baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan Fc hapo jana
Mchezo wa marudiano utapigwa Septemba 17 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE