Kukosa penati kusituvuruge - Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2018
Kukosa penati kusituvuruge - Lwandamina
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema hakuna haja ya mshambuliaji kinara wa mabao Obrey Chirwa kulaumiwa kwa kukosa mkwaju wa penati kwa kuwa tukio hilo ni sehemu ya mchezo.

Kumekuwa na mjadala mpana miongoni mwa mashabiki wa Yanga kwenye mitandao ya kijamii wakilitaka benchi la ufundi lifikirie kukabidhi majukumu ya upigaji wa penati kwa mchezaji mwingine baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa Chirwa.

Licha ya kuwa mchezaji tegemeo kikosini, takwimu zake za hivi karibuni kwenye upigaji wa mikwaju ya penati sio za kuridhisha kwani kati ya penati tano, Chirwa amekosa tatu na kufunga mbili.

Lakini kocha Lwandamina amesema hiyo sio sababu ya kumfanya Chirwa ashambuliwe kwani tangu ajiunge na Yanga amefunga penati nyingi pia.

"Ametufungia penati nyingi sana na muhimu lakini kwa sababu jana (juzi) alikosa penalti ndiyo tumhukumu?" alihoji Lwandamina.

"Haiwezekani kufanya hivyo, jambo kubwa na la msingi tuendelee kuwaunga mkono wachezaji wetu ili waongeze juhudi za kupambana uwanjani ili tuweze kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa marudiano."

Yanga imerejea kujifua leo tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18 dhidi ya Majimaji utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa (au Uhuru) keshokutwa Jumatano.

Baada ya mchezo huo itasafiri kwenda Shelisheli kuivaa St Louis ukiwa ni mchezo wa marudiano wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Yanga inahitaji sare au ushindi pia hata ikifungwa kwa tofauti ya bao moja (ukiondoa matokeo 1-0) itasonga mbele.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’