Tuko tayari kuwakabili Mtibwa Sugar - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Sep 2022
Tuko tayari kuwakabili Mtibwa Sugar - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Nabi amesema wataingia katika mchezo huo kwa kuwaheshimu Mtibwa Sugar kwani wana timu nzuri

"Tunawaheshimu Mtibwa Sugar, wamekuwa na msimu mzuri kwa kuangalia nafasi wanayoshika kwenye msimamo wa ligi. Hata hivyo dhamira yetu ni kuona tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo," alisema Nabi

Akizungumzia hali ya kikosi, Nabi amesema mlinda lango Djigui Diarra atakosekana kwenye mchezo huo akiendelea kupona majeraha aliyopata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union

Aidha wachezaji Farid Mussa na Salum Abubakar 'Sure Boy' nao wamepona majeraha yaliyowafanya wakose mechi zilizopita huenda wakawa na nafasi ya kutumika hapo kesho

Winga Bernard Morrison nae afya yake imeimarika na watamuangalia kwenye mazoezi ya mwisho leo kuona kama wanaweza kumtumia

Nabi amesema benchi la ufundi limewahasisha wachezaji kujituma kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa mgumu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’