Kambole atakuwa nje muda mrefu - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2022
Kambole atakuwa nje muda mrefu - Nabi

Jana katika Mkutano na Wanahabari, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alitoa ufafanuzi kukosekana kwa mshambuliaji Lazarus Kambole ambaye tangu aliposajiliwa na Yanga hajacheza mechi yoyote ya kimashindano

Nabi alibainisha kuwa Kambole ni majeruhi licha ya kufanya mazoezi na wenzake, hayuko timamu kuweza kucheza mechi za mashindano

Aidha Nabi alithibitisha kuwa usajili wa winga Tuisila Kisinda ulikuwa maalum kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kambole na kuwa Mzambia huyo angeendelea kuimarika na pengine atakapokuwa fit wataweza kumjumuisha kikosini

"Natambua uongozi ulimsajili Kisinda (Tuisila) kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kambole ambaye hawezi kucheza sasa kwa sababu ni majeruhu. Viongozi waliandika barua TFF kuomba mabadiliko ya mchezaji huyo hivyo tunasubiri," alisema Nabi

Hata hivyo taarifa ambayo bado sio rasmi ni kuwa Yanga italazimika kusubiri kumsajili Kisinda kwenye dirisha dogo baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kubariki uamuzi wa TFF kumzuia Kisinda kuitumikia Yanga wakati huu kwa madai kuwa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji 12 wa kigeni

Taarifa iliyotolewa na TFF wiki iliyopita ilibainisha kuwa, wakati Yanga ikikamilisha usajili wa Kisinda kutoka RS Berkane, tayari TFF ilikuwa imewasilisha majina ya wachezaji 12 wa kigeni wa Yanga kwa shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) na kupatiwa leseni zao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’