Ngoma ameikumbusha Yanga umuhimu wa kufanya usajili kwa makini

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
12 Feb 2018
Ngoma ameikumbusha Yanga umuhimu wa kufanya usajili kwa makini
Usajili wa Donald Ngoma ni moja ya usajili uliokosa umakini kuwahi kufanywa na klabu ya Yanga.

Licha ya kuwa tishio katika msimu wake wa kwanza akiwa Yanga, Ngoma msimu wake wa pili haukuwa mzuri baada ya kukumbwa na majeruhi mfululizo.

Katika msimu wa 2016-17, Ngoma hakucheza mchezo wowote kwenye mzunguuko wa pili, ligi kuu ya Vodacom licha ya kufunga mabao nane katika mzunguuko wa kwanza.

Wakati hatma yake ikiwa bado haijawekwa wazi, uko uwezekano mkubwa Yanga itavunja mkataba wake baada ya kubaini majeraha yake si ya kupona leo wala kesho.

Ngoma anasumbuliwa na majeraha sugu ya goti, nyama za paja (misuli) na kisigino.

Ngoma amekuwa akienda kwao Zimbabwe kutibiwa mara kwa mara akidai kuwa na daktari wake maalumu anayeyafahamu vyema matatizo yake.

Lakini baada ya Yanga kufanya uchunguzi wa swala hilo kupitia Kamati waliyounda, imebaini kuwa huenda Ngoma alikuwa akificha uhalisia wa majeraha yake kwa kuogopa kuvunjiwa mkataba wake mnono.

Ngoma ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mnono kwenye kikosi cha Yanga.

Moja ya makosa yaliyofanywa na Kamati ya usajili ya Yanga ni kutojiridhisha juu ya utimilifu wa afya yake kabla ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Ifahamike alirejea Yanga baada ya zaidi ya miezi minne kutoonekana ikielezwa alikuwa Afrika Kusini kutibiwa majaraha yake.

Ilikuwa vyema kwa uongozi wa Yanga kumfanyia vipimo vya Afya kuhakikisha yuko timilifu kwa kuwa tayari alishakosa nusu msimu kutokana na majeraha.

Kosa kama hilo pia lilifanywa kwa Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko ambao nao walisaini mikataba ya miaka miwili halafu baada ya muda mfupi wakarejea kitandani kuuguza majeraha.

Watatu hao msimu huu hawajaisaidia Yanga licha ya kuwa wachezaji ghali na waliokuwa wanategemewa.

Wakati Tambwe na Kamusoko ikielezwa kuwa wako tayari kurejea dimbani, Ngoma imebainika kuwa sio wa kupona leo wala kesho, Yanga haina namna zaidi ya kuvunja mkataba wake.

Kama si hivyo italazimika ikubali kuendelea kuingia hasara ya kumhudumia mchezaji ambaye haifahamiki atarejea lini dimbani.

Lakini hasara hii isingetokea kama angefanyiwa uchunguzi wa kina kabla hajakabidhiwa mkataba mpya.

Ni wakati muafaka sasa kwa vilabu vyetu kuiga utaratibu wa usajili barani Ulaya na kwingineko kwamba kabla ya kusajiliwa mchezaji lazima afuzu vipimo vya afya.

Vinginevyo tutaendelea kusajili wachezaji kwa gharama kubwa halafu wanacheza mechi moja, mbili, tatu kisha wanarudi kitandani kuuguza majeraha.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’